MAGOLI YOTE: MWADUI FC 1-2 YANGA SC (TPL – 22/11/2018)

Опубликовано: 22 Ноябрь 2018
на канале: Azam TV
239,334
541

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC leo wamepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo wao wa kwanza nje ya Dar es Salaam kwenye ligi msimu huu, na kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo wowote hadi sasa.

Yanga ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 10 kupitia kwa Heritier Makambo, kabla ya Mwadui kusawazisha dakika ya 40 kupitia kwa Salim Aiyee akitumia makosa ya kipa wa Yanga Klaus Kindoki, lakini mkongwe Mrisho Ngasa akaamua matokeo kwa kuifunga Yanga bao la pili dakika ya 58.
Katika mchezo huu kocha wa Yanga Mwinyi Zahera alilazimika kufanya mabadiliko kwa kumuweka nje kipa Klaus Kindoki na nafasi yake ikachukuliwa na Ramadhan Kabwili, Amissi Tambwe nafasi yake ikachukuliwa na Raphael Daud, na Gadiel Michael nafasi ikachukuliwa na Pato Ngonyani.
Matokeo haya yanaifanya Yanga kupanda hadi nafasi ya pili ikifikisha pointi 29 katika michezo 11 iliyocheza ambapo imetoka sare michezo miwili na kushinda michezo tisa.


Смотрите видео MAGOLI YOTE: MWADUI FC 1-2 YANGA SC (TPL – 22/11/2018) онлайн, длительностью часов минут секунд в хорошем качестве, которое загружено на канал Azam TV 22 Ноябрь 2018. Делитесь ссылкой на видео в социальных сетях, чтобы ваши подписчики и друзья так же посмотрели это видео. Данный видеоклип посмотрели 239,334 раз и оно понравилось 541 посетителям.