Nyimbo za Sayansi! | Ubongo Kids - elimu burudani wa watoto

Published: 23 June 2017
on channel: Ubongo Kids Kiswahili
4,734,783
6.8k

Imba nyimbo za sayansi na wakina Mama Ndege, Anko T, Kibena, Kiduchu, Koba, Baraka na Amani! Jifunze kuhusu nishati ya sauti, mwanga, mwili, ukuaji, uzito na ujazo kupitia nyimbo za Ubongo Kids!

--

Jamani! Mwaka huu, Ubongo Kids ni ZAIDI ya hisabati na sayansi! Msimu huu si KAMA ULIVYOZOEA!

Ubongo Kids MPYA inamjenga mwanao, ikimpa fikra komavu zitakazomwezesha kutambua kusudi lake masomoni na maishani!

Njoo nasi Kokotoa, ukajifunze kutumia uwezo na utashi wako kusuluhisha changamoto zinazokukabili ili ufike pale utakapo!

Msimu wa 3 wa Ubongo Kids utakuandaa kifikra, ukichochea uwezo wako wa kung’amua matatizo na kuyatafutia ufumbuzi.

Ubongo Kids ni mfululizo wa hadithi za kusisimua zilizo katika mfumo wa elimu-burudani kwa ajili ya watoto wa miaka 7 hadi 13, zikitumia nyimbo na maudhui ya Kiafrika kuwafundisha hisabati na sayansi!

Katuni hii mahususi ya elimu inaandaliwa na Ubongo Learning, ambao pia ni watengenezaji wa kipindi murua ya AkiliandMe inayowaandaa watoto wa miaka 3-6 kwa ajili ya kwenda shule!

Tazama Ubongo Kids kila Jumamosi na Jumapili saa 3 asubuhi kupitia TBC1! Pata pia webisodes zetu zote kupitia: http://www.ubongokids.com


Watch video Nyimbo za Sayansi! | Ubongo Kids - elimu burudani wa watoto online, duration hours minute second in high quality that is uploaded to the channel Ubongo Kids Kiswahili 23 June 2017. Share the link to the video on social media so that your subscribers and friends will also watch this video. This video clip has been viewed 4,734,783 times and liked it 6.8 thousand visitors.